KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 17, 2012

Mhariri wa Habari Jambo Leo afariki dunia hotelini Morogoro

Mhariri wa habari wa gazeti la Jambo leo, Willy Edward amefariki dunia chumbani kwake katika hoteli aliyofikia mjini Morogoro.

Habari za kusikitisha zilizotua katika mtandao wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/ asubuhi hii kutoka mkoani Morogoro zinaeleza kuwa Willy alikuwepo mkoani Morogoro katika mafunzo ya siku moja pamoja na wanahabari wengine na kwamba inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu kwa muda mrefu.

Akithibitisha juu ya taarifa hiyo, mhariri wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kulwa Karedia ambaye walikuwa wote na Willy mjini Morogoro amesema kuwa, hadi saa tatu usiku walikuwa wote na baada ya hapo aliwaaga wanahabari wenzake kuwa anakwenda kulala .

Kwa upande wake mpasha taarifa wa kwanza kabisa katika mtandao huu, Dotto Mwaibale alisema kwa njia ya simu kwa kutumia maneno machache sana kuwa mzee wa matukio umepata taarifa kuwa Willy Edward Amefariki Morogoro?

Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Nevelin Meena alieleza kusikitishwa na kifo cha mhariri mwenzao huyo na kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa juu ya kifo hicho.

Mtandao huu jana majira ya saa 11 jioni ulipata kuzungumza na Willy Edward kwa mara ya mwisho kwa njia ya simu ambapo alitaka kujua zaidi juu ya kile alichozungumza katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa Nape Nauye akiwa ziarani wilayani Kilolo ili awasiliane na ofisi yake wapate kuitumia katika gazeti la Jambo leo la Leo. Habari hiyo imetumika ikiwa na kichwa cha habari 'Nape awaonya makandarasi Kilolo'.

Nukuu ya willy Edward jana katika mazungumzo yetu kwenye simu:

Mzee wa matukio daima Mambo vipi ?Nimesoma katika mtandao wako juu ya ziara ya Nape Kilolo sasa nitampigia simu mhariri wa habari Jumapili, Said Mwishehe ama Beny Kisaka ili aweze kuitumia habari hiyo kwani nimeipenda sana jinsi ambavyo Nape alivyogeuka mwiba kwa kupigania ajira za vijana ...mimi nipo Morogoro katika semina mara moja kesho nitageuza Dar ... wasalimie rafiki zangu Salim Asas na Daud Yassin. Muulize pia Yassin vipi mwaka huu kombe la Muungano Mufindi alicheka ha ha ha na kukata simu.

Mpenzi mdau wa mtandao huu habari zaidi juu ya kifo cha Willy Edward utaendelea kuzipata zaidi katika mtandao endelevu wa Iringa wa http://www.francisgodwin.blogspot.com/

Sote tulimpenda sana Willy Edward ila Mungu kampenda zaidi yetu hivyo jina lake Mungu na lihimidiwe zaidi .Amina

No comments:

Post a Comment