KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 24, 2012

Kigi Makasi aanza kuonyesha cheche zake Simba

Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Simba leo wamelazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 na Express ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ya soka iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Mechi hiyo ilikuwa ya pili kwa Simba katika ziara yake ya mechi za kirafiki katika mikoa ya kanda ya ziwa. Katika mechi yake ya kwanza jana, Simba iliichapa Toto African mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Kiungo mpya wa Simba, Kiki Makasi aliyesajiliwa kutoka Yanga alianza kuonyesha cheche zake akiwa ndani ya uzi mweupe na mwekundu baada ya kuifungia Simba bao la kuongoza dakika ya 20.

Hata hivyo, Express ilisawazisha bao hilo dakika ya 40 mfungaji akiwa Joseph Kaira. Hadi pambano hilo lilipomalizika, timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka sare hiyo ya mabao.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic anatarajiwa kutua nchini leo alfajiri akitokea nyumbani kwao Serbia alikokwenda kwa mapumziko.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jana kuwa, kocha huyo atawasili saa 8:45 usiku kwa ndege ya shirika la ndege la Uturuki na anatarajiwa kuanza kibarua chake baada ya timu hiyo kurejea kutoka Mwanza na Shinyanga.

No comments:

Post a Comment