KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 24, 2012

MICHAEL ESSIEN ARUDIANA NA NADIA BUARI











Wapenzi wa zamani, mwanasoka Michael Essien na mcheza filamu, Nadia Buari wametangaza kurejesha rasmi uhusiano wao wa kimapenzi, ambao ulikufa miaka michache iliyopita.

Essien na Nadia walitangaza kurejesha uhusiano huo wiki iliyopita katika pati maalumu iliyofanyika kwenye hoteli moja maarufu ya mjini Accra, Ghana.

Katika pati hiyo ya nguvu, lakini iliyohudhuriwa na watu wachache, Essien na Nadia walipeana mabusu babu kubwa, yanayojulikana kwa majina ya 'nakupenda', 'nimekumisi', 'nakuhitaji', 'hakuna mwingine zaidi yako' na mengineyo kadhaa.

Kwa mujibu wa mtandao wa Ghana Celebrities, wawili hao wameamua kuzika tofauti zao zilizosababisha mapenzi kati yao kufa miaka miwili iliyopita.

Essien, kiungo nyota wa klabu ya Chelsea ya England na Nadia walifanya pati hiyo kwenye ukumbi wa Villaggio Primavera, ambapo pia walihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha Diva Show, Nana Aba Anamoah.

No comments:

Post a Comment