KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, June 5, 2012

KIGOGO WIZARA YA NISHATI AWANIA UONGOZI YANGA

KATIBU wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakhim Masu leo asubuhi amechukua fomu ya kugombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.

Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili amewataja wengine waliochukua fomu leo ni Mussa Katabaro, Muzamil Katunzi, Lameck Nyambaya, Edgar Fongo, Ahmad Waziri Gao na Yona Kevela.

Mapema jana, vigogo wengine watatu walichukua fomu za kugombea nafasi tofauti, hivyo kufanya uchaguzi wa Yanga utakaofanyika Julai 15, mwaka huu uzidi kuwa na msisimko.

Waliochukua jana ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, milionea Abdallah Ahmed Bin Kleb na kigogo wa zamani wa Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, Isaac Chanji.

Lakini kuna uvumi kwamba na milionea Yussuf Manji amechukua fomu ya kuwania Uenyekiti, ingawa Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili anaendelea kukataa kwamba amechukua.

Idadi ya waliochukua fomu hadi sasa inafika watu 11, baada ya awali Ayoub Nyenzi kuchukua fomu ya kugombea Makamu Mwenyekiti, Jumanne Mwamenywa, John Jambele, Peter Haule, Gaudicius Ishengoma, Abdallah Sharia na Saleh Abdallah, wote Ujumbe.

Uchaguzi wa Yanga unaokuja baada ya Wajumbe wengi wa Kamati ya Utendaji iliyoingia madarakani mwaka juzi, kujiuzulu akiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga na mwisho wa zoezi la kuchukua ni kesho, wakati kurudisha ni kesho saa 10:00 jioni na usaili ni Juni 19, mwaka huu.

Kaswahili amesema kesho ikifika saa 10:01 hatapokea fomu wala kutoa fomu, kwani saa 10:00 ndio mwisho wa kurudisha fomu kwa wagombea wote.

No comments:

Post a Comment