KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, June 8, 2012

Z'BAR YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA

TIMU ya soka ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, imefanikiwa kutinga nusu fainali
ya michuano ya Kombe la Dunia kwa nchi zisizo wanachama wa Shirikisho la
soka la Kimataifa (Fifa), inayoendelea nchini Kurdistan.

Baada ya Heroes kuanza kwa kishindo michuano hiyo kwa ushindi wa 6-0
dhidi ya Latia, juzi usiku walivuna ushindi wa pili wa mabao 3-0 dhidi ya Tamil Elaam kwenye uwanja wa Erbir.

Kwa ushindi huo, Heroes chini ya Kocha Mkuu wake Hemed Moroko,
wamemaliza vinara katika kundi lao la B, lililokuwa na timu tatu, ikiwemo
Ratia.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Chama cha soka cha Zanzibar (ZFA), Munir
Zacharia, Heroes wamekuwa gumzo kwenye michuano hiyo maarufu kwa jina
la Viva World Cup.

Heroes walianza kupata bao la kwanza dakika ya 22, likifungwa na Khamis
Mcha, ambalo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kiliendelea kuwa kizuri kwa Heroes, kwani dakika ya 61,
walifunga bao la pili likipachikwa wavuni na Amir Hanad kabla ya Awadh
Juma kufunga la tatu dakika ya 90.

Katika hatua ya nusu fainali, Heroes leo itacheza na Cyprus iliyotoka kundi C,
ambayo ilisonga mbele licha ya kufunga mabao 2-1 na Province ya Ufaransa.

Mechi nyingine ya nusu fainali, itawakutanisha wenyeji wa michuano hiyo
Kurdistan dhidi ya Province, itakayochezwa leo usiku huku fainali ikichezwa
kesho.

Kocha Moroko wa Zanzibar Heroes, amesema kikosi chake kipi fiti kukabiliana
na ushindani wa leo, akitaka kutinga fainali na ikiwezekana kurejea na
ubingwa.

Heroes wamekwenda huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo,
Said Ali Mbarouk, akiahidi shilingi mil 18 kama wakitwaa ubingwa na nusu
yake, wakinusa fainali.

No comments:

Post a Comment