KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, June 8, 2012

Mwasikili kutua Bongo J'pili

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ Sophia Mwasikili anatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa tayari kwa mchezo baina ya timu hiyo na Ethiopia utakaopigwa juni 16 mwaka huu.


Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) ni mahususi kwa ajili ya kuwania tiketi ya kucheza fainali zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.

Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura amesema leo kwamba awali nyota huyo anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Luleburgargusu ya Uturuki awali ilikuwa atue nchini jana lakini ilishindikana baada ya kuchelewa ndege.

Alisema benchi la ufundi bado linamuhitaji mchezaji huyo kutokana na mchango wake katika kikosi hicho kilichopo kambini katika hosteli ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kibaha, Pwani kikiendelea na maandalizi yake ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment