KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 7, 2012

DESMOND: Nataka watoto wangu wajue baba yao alikuwa maarufu

LAGOS, Nigeria
MSANII nyota wa filamu wa Nigeria, Desmond Elliot amesema anataka watoto wake wawe na kumbukumbu ya umaarufu wakekatika tasnia ya filamu.
Desmond amesema hayo kupitia mahojiano aliyoyafanya na jarida la mwezi huu la Genevieve, linalomilikiwa na Betty Irabor.
Katika jarida hilo linalotoka kila mwezi, Desmond ameelezea kwa kirefu kuhusu maisha yake, alivyojitosa katika fani hiyo, matatizo aliyokumbana nayo na mafanikio aliyoyapata hadi sasa.
Katika ukurasa wa mbele wa jarida hiyo, kumewekwa picha kubwa ya Desmond akiwa na mkewe na watoto wao wanne.
Mbali na kucheza filamu mbalimbali, Desmond kwa sasa pia ni mtayarishaji na muongozaji wa filamu.
Desmond alianza kujipatia umaarufu kupitia tamthilia ya Everyday People, ambayo ilimshirikisha msanii nyota wa zamani wa fani hiyo nchini Nigeria, marehemu Sam Loco Efe.
Tangu wakati huo, ameshiriki kucheza filamu nyingi na kuwa kivutio kama ilivyo kwa Jim Iyke, Ramsey Nouah na wengineo.

No comments:

Post a Comment