KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 7, 2012

D'Banj akerwa kuzushiwa kifo

LAGOS, Nigeria
MWANAMUZIKI nyota wa Nigeria, Dapo Oyebanjo, maarufu zaidi kwa jina la D’Banj, amewajia juu watu wanaozusha taarifa mbaya dhidi yake.
D’Banj amesema watu hao hawamtakii mema na wala kupenda maendeleo yake ndiyo sababu kila kukicha wamekuwa wakimzushia tuhuma mbalimbali.
Mwanamuziki huyo nyota wa Nigeria amesema hayo, kufuatia uvumi uliosambazwa hivi karibuni kwamba amekufa.
Ilidaiwa kuwa, mwimbaji huyo wa miondoko ya ‘Oliver twist‘ alipigwa risasi na kufa na watu watatu waliokuwa na silaha mjini Atlanta, Marekani baada ya kutoka kwenye studio za Kanye West.
“Hizi ni hisia za watu wasionitakia mema,”alisisitiza mwanamuziki huyo mwenye kipaji cha aina yake.
D’Banj amewaelezea watu hao kuwa ni wenye nyoyo za chuki dhidi yake na kusisitiza kwamba, kamwe hawawezi kufanikiwa kwa wayatakayo.
Alisema haelewi ni kwa nini watu hao wamekuwa wakimzushia kifo mara kwa mara na kuwataka waache tabia hiyo mara moja.
“Nawaomba muupuuze uzushi huo. Mimi nipo hai na hali yangu ni nzuri. Namshukuru Mungu. Nawashukuru wale wote walioonekana kuguswa na taarifa hizo za uzushi,”alisema.

No comments:

Post a Comment