KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, June 4, 2012

Twanga Pepeta yapata viongozi wapya

UONGOZI wa Kampuni ya African Stars Entertainment (ASET) imefanya mabadiliko kadhaa ya uongozi katika bendi yake ya Twanga Pepeta International. Mabadiliko hayo yalitangazwa jana na Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka alipokutana na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar es Salaam.

Katika mabadiliko hayo, Asha alimtangaza Muddy Pizzaro kuwa ndiye msemaji mpya wa bendi, Muddy K anakuwa meneja matukio wakati Omary Baraka anaendelea kuwa mkurugenzi mtendaji.

Katika mabadiliko hayo, Amigolas anakuwa meneja wa bendi, Luiza Mbutu anaendelea kuwa kiongozi wa bendi akisaidiwa na Saleh Kupaza.

Kiongozi wa wanenguaji anaendelea kuwa Maria Salome kwa wanawake na kwa wanaume anaendelea kuwa Sidy Boy.

No comments:

Post a Comment