KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 7, 2012

Ronaldo anogewa Madrid

WARSAW, Poland
MCHEZAJI nyota Cristiano Ronaldo amesema anataka kustaafia soka Real Madrid baada ya kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Hispania msimu huu.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 27 usajili wake ulivunja rekodi duniani kufuatia kununuliwa kwa dau la pauni milioni 80 (sasa sh bilioni 200) kutoka Manchester United, ambapo katika ligi ya msimu uliopita alifunga mabao 46 na Real kuivua ubingwa Barcelona baada ya kuufukuzia miaka minne.

Amesema kuwa, bila kificho anapenda kubaki Real Madrid maisha yake yote."Hata leo naweza kusaini mkataba wa miaka 10, lakini inategemea na mambo mengine," alisema.

Ronaldo, ambaye amefunga mabao 55 katika mechi 60 za mashindano yote iliyocheza Real Madrid msimu uliomalizika mwezi uliopita, alikiri kuwa bado ana deni la kuilipa klabu hiyo ya Hispania iliyomnunua kwa fedha nyingi miaka mitatu iliyopita.

Aliongeza: "Yote niliyofanikiwa nimefanya kwa kuvuja jasho na kipaji changu, lakini kwa ujumla ni kazi kubwa. Hakuna kinachoshindikana chini anga.

"Kwa sasa nafikiria jinsi nilivyo bado mchezaji niliyesajiliwa kwa dau kubwa katika historia ya soka na siku zote najaribu kudhihirisha ubora uwanjani kutokana na kamari iliyocheza klabu kwangu."

Ronaldo, ambaye yupo na kikosi cha Ureno kinachoshiriki michuano ya Euro 2012, pia amefurahishwa na uamuzi wa Mreno mwenzake kocha Jose Mourinho kuongeza mkataba mpya unaombakisha Santiago Bernabeu mpaka 2016.

Akihojiwa na gazeti la Hispania la Marca, aliongeza: "Nina furaha Mourinho anabaki. Klabu kama Real Madrid inastahili kuwa na kocha bora kama (Jose) Mourinho. Kocha ameamua kubaki. Ninavyoona ni kwamba Real Madrid haiwezi kutwaa mataji bila ya kuwepo Mourinho katika benchi."

No comments:

Post a Comment