KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 7, 2012

Boateng abambwa na kidosho hotelini




BERLIN, Ujerumani

LICHA ya Ujerumani kukabiliwa na mechi ya ufunguzi dhidi ya Ureno Jumamosi katika mashindano ya Euro 2012, mchezaji Jerome Boateng amebambwa na mrembo kwenye hoteli isiyo na hadhi.Mwanasoka huyo wa zamani wa Manchester City, ambaye sasa anakipiga Bayern Munich, aliingia hotelini mjini Berlin na mrembo Gina-Lisa Lohfink juzi usiku bila ya kujali jukumu lililopo mbele yao katika kivumbi cha Ulaya.Boateng mwenye watoto wawili alizua walakini baada ya kukutwa na mrembo huyo aliyewahi kucheza picha za utupu.Gina alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo alisema: “Jerome alikutana na mimi kwa nia ya kufahamiana. Tulikutana baa hotelini kwangu mida ya saa 8 usiku. Tuliingia chumbani kwangu lakini tulizungumza tu.”

No comments:

Post a Comment