KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 7, 2012

Genevieve apata mkataba mnono wa Range Rovers

LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu nyota wa Nigeria, Genevieve Nnaji ameingia mkataba mnono wa mamilioni ya pesa na kampuni moja ya magari nchini humo.
Kwa mujibu wa mtandao wa naijerules, Genevieve ameingia mkataba huo na Kampuni ya Coscharis Motors kwa ajili ya kutangaza magari aina ya Range Rovers.
Kampuni ya Coscharis ndiyo inayomiliki aina hiyo ya magari nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa mkataba huo, Genevieve atakuwa akilipwa dola 100,000 za Uingereza katika miezi sita ya kwanza.
Habari za uhakika zilizonaswa na mtandao huo zimeeleza kuwa, mkataba huo utadumu kwa miezi 12, lakini upo wazi kuongezwa iwapo yatafikiwa makubaliano.
Genevieve amepewa mkataba huo na Coscharis baada ya kumpiku mwigizaji mwingine nyota wan chi hiyo, Desmond Elliot.
Chanzo cha habari kimeueleza mtandao huo kuwa, wataalamu wa kampuni hiyo walikuwa na wakati mgumu wa kumchagua yupi kati ya Genevieve na Desmond apewe mkataba huo.
Kuna habari kuwa, Genevieve alipewa nafasi hiyo kutokana na umaarufu wake, ikilinganishwa na Desmond.
“Genevieve ameonekana kuwa ni maarufu na mwenye mafanikio zaidi katika kutangaza bidhaa mbalimbali kuliko Desmond,” kilieleza chanzo hicho cha habari.

No comments:

Post a Comment