KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 7, 2012

Wazimbabwe kuchezesha Taifa Stars na Gambia

Waamuzi kutokaZimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua
ya makundi Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia
itakayochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mwamuzi wa
kati atakuwa Ruzive Ruzive. Waamuzi wasaidizi ni Salani Ncube na Edgar
Rumeck wakati mwamuzi wa akiba ni Norman Matemera.
Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Fanie Wallace
Mabuza kutoka Swaziland wakati mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni
Ali Baligeya Waiswa.
Waamuzi hao watawasili nchini kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa
ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo
hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya South African Airways. Mtathmini wa
waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya
Airways.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na
mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya
Kocha Mkuu Kim Poulsen.
GAMBIA KUWASILI LEO USIKU

Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa iwasili nchini leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
The Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini
kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya
ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.
Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza mpira
wa kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa
Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo.
Wachezaji walioko katika msafara huo ni Musa Camara, Abdou Jammeh,
Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou
Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay na Demba Savage.
Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou
Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa,
Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum
Faal.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA
IJUMAA JUNI 8

01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume10.00 jioni
Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9

04.00 asubuhi Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi
wa TFF

10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa

No comments:

Post a Comment