KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, July 2, 2012

Yanga yapeleka yosso Zanzibar

KLABU ya Yanga imepeleka kikosi cha pili, katika michuano ya ujirani iliyoanza
jana visiwani Zanzibar.
Awali, uongozi wa Yanga uligoma kupeleka timu Zanzibar kushiriki michuano
hiyo kwa madai ya kuhofia wachezaji wake kuumia kabla ya kuanza Kombe la
Kagame Julai 14.
Timu hiyo iliondoka saa 10:30 jioni ikiwa na wachezaji wa kikosi cha pili huku
wachezaji wake nyota wakiendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Kaunda,
Dar es Salaam.
Michuano ya Kombe la Kagame inaanza Julai 14 hadi 28 kwenye uwanja wa
Taifa na Chamazi, Dar es Salaam ambapo Yanga ndio mabingwa watetezi.
Mazoezi ya jana yalinogeshwa na kiungo nyota wa kimataifa wa Rwanda
Haruna Niyonzima aliyetua nchini juzi akitokea nyumbani kwao kwa
mapumziko.
Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa, alisema waliokwenda Zanzibar ni
wachezaji wa Yanga na alikanusha kuwa klabu hiyo imepeleka kikosi cha pili.
"Nipo katika mkutano, lakini kama ni timu ipi inakwenda Zanzibar ukweli ni
kwamba wote ni wachezaji wa Yanga taarifa kuwa tumepeleka B si sahihi,"
alisema Mwesigwa.
Yanga ilicheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki wa kimataifa kujiandaa na
msimu ujao ambapo ilishinda mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Uganda
Express.
Michuano hiyo inashirikisha timu nane ambazo ni Yanga, Simba na Azam
kutoka Tanzania Bara na kutoka Zanzibar ni Mafunzo, Jamhuri, Super Falcon,
Karume Boys na Zanzibar All Stars.

No comments:

Post a Comment