KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, July 12, 2012

Ray aibuka na filamu mpya ya Mfungo wa Ramadhani

MSANII nyota wa filamu nchini, Vicent Kigosi ‘Ray’ ameibuka na filamu mpya inayojulikana kwa jina la The Glory of Ramadhani.
Ray amesema kupitia blogu yake ya thegreatest kuwa, filamu hiyo imelenga kufikisha ujumbe kwa waumini wa dini ya kiislamu kuhusu mfungo wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa Ray, filamu hiyo itawawezesha watu mbalimbali kujifunza mambo mazuri ya kumpendeza Mungu, hasa wakati wa mfungo wa Ramadhani.
“Filamu hii si ya kuikosa, ni mahususi kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani,”ameeleza Ray kupitia blogu yake hiyo.
Ray alisema filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni siku tatu kabla ya kuanza kwa mwezi wa Ramadhani.
Msanii huyo amedokeza kuwa, ameamua kutunga filamu hiyo kwa kuzingatia kuwa, sio waislamu wote wanaokwenda msikitini kwa ajili ya kufanya ibada na kusikiliza mawaidha.
“Tumeitengeneza filamu hii kwa umakini mkubwa, lengo ni kuwafundisha watu kwamba wanatakiwa kutenda mema miezi yote kumi na mbili na sio mwezi mmoja,”alisema.
Ray ni mmoja wa wasanii wanaoongoza nchini kwa kutunga filamu nyingi, akiwa anachuana na marehemu Steven Kanumba.
Miongoni mwa wasanii walioshiriki kucheza filamu hiyo ni pamoja na mwanadada Neshi, Chuchu Hans, Bachard na Abdalla Ramadhani ‘Dula’.

No comments:

Post a Comment