KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, July 7, 2012

WASANII BORA ZANZIBAR WAPATA TUZO

Mkurugenzi wa redio ya Briz FM, Mariam (kushoto), akimkabidhi tuzo ya kuwa msanii bora wa kike wa muziki wa Afro Pop, msanii Baby J, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa tuzo za wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.

Mwakilishi wa Jimbo la Raha Leo, Salim Nassor akimkabidhi tuzo ya msanii bora chipukizi wa mwaka, msanii Emma Score wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa tuzo hizo za wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.

Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya Zenji FM, Mohamed Seif Khatib, akimkabidhi tuzo msanii, Rukia Ramadhan, aliyeibuka mshindi kwa kuwa mwimbaji bora wa mwaka wa Taarab Asilia wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa tuzo za wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment