KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, July 15, 2012

MANJI MWENYEKITI MPYA YANGA

UCHAGUZI mdogo wa klabu ya Yanga ulimalizika usiku wa kuamkia leo kwa mfadhili wa klabu hiyo, Yussuf Manji kuchaguliwa kuwa mwenyekiti.

Manji alishinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 1876, ambazo ni sawa na asilimia 97 ya kura zilizopigwa.

Manji alifuatiwa na John Jambele aliyeambulia kura 40, ambazo ni sawa na asilimia 2.6 wakati Rdgar Chibura aliambulia kura nne ambazo ni sawa na asilimia 0.24.

Nafasi ya makamu mwenyekiti ilichukuliwa na Clement Sanga, aliyepata kura 1948, ambazo ni sawa na asilimia 62.6.

Sanga aliwabwaga Yono Kevella, aliyepata kura 475, sawa na asilimia 23 wakati Ayubu Nyenzi alipata kura 288, ambazo ni sawa na asilimia 14.

Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa kamati ya utendaji ni Abdalla Bin Kleb (kura 1942), Mussa Katabalo (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922) na George Manyama (kura 682).

No comments:

Post a Comment