KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, July 9, 2012

SIMBA, AZAM KUCHEZA FAINALI KOMBE LA URAFIKI



TIMU za soka za Simba na Azam zimefuzu kucheza fainali ya
michuano ya Kombe la Urafiki baada ya kuibuka na ushindi dhidi
ya Super Falcon na Zanzibar All Stars.
Katika mechi hizo za nusu fainali zilizochezwa jana kwenye
Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Simba iliichapa All Stars bao 1-0
wakati Azam iliichapa Super Falcon mabao 2-0.
Kwa ushindi huo, Simba na Azam sasa zitakutana katika fainali ya
michuano hiyo itakayochezwa kesho kwenye uwanja huo.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Tcheche ndiye
aliyeibeba Azam baada ya kuifungia mabao yote mawili katika
kipindi cha pili.
Tcheche alifunga bao la kwanza dakika ya 67 baada ya
kuunganisha wavuni krosi kutoka Hamisi Mcha kabla ya kuongeza
bao la pili kwa njia ya penalti dakika ya 77 baada ya Samir Haji
Nuhu kuangushwa na beki Samir Saidi ndani ya eneo la hatari.
Azam ililazimika kumaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji 10 baada
ya mshambuliaji wake, Gaudence Mwaikimba kutolewa nje kwa
kadi nyekundu dakika ya 54 kwa kosa la kumpiga kiwiko Abdul
Ally.
Nayo Simba ilijipatia bao lake la pekee na la ushindi kupitia kwa
mshambuliaji Kani Mbiyavanga. Alifunga bao hilo dakika ya 57
baada ya kuunganisha krosi kutoka kwa Felix Sunzu, aliyeingia
kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Salim Kinje,
All Stars ilifanikiwa kuzitikisa nyavu za Simba dakika ya 85 kwa
bao lililofungwa na Sabri Ramadhani China, lakini lilikataliwa na
mwamuzi kwa madai kuwa mfungaji alikuwa ameotea.

No comments:

Post a Comment