KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, July 8, 2012

FAMILIA YA SERENA YATAMBA WIMBLEDON

Serena na Venus wakiwa na vikombe walivyotwaa katika michuano ya wazi ya tennis ya wachezaji wawili wawili ya Wimbledon

Serena na Venus wakipongezana na wapinzani wao baada ya mchezo kumalizika

Serena akirudisha mpira kwa nguvu kwa mpinzani wake wakati wa fainali ya mchezaji mmoja mmoja

Serena akipongezwa na baba yake, Richard William mara baada ya kutwaa taji la mchezaji mmoja mmoja. Kushoto ni dada yake, Venus

Serena akishangilia kwa kulala uwanjani baada ya kushinda taji la tennis la Wimbledon

Serena akinyanyua juu tuzo aliyozawadiwa baada ya kushinda taji la tennis la Wimbledon


Saa chache baada ya kutwaa taji la michuano ya wazi ya tennis ya Wimbledon kwa mchezaji mmoja mmoja, Serena Williams alifanikiwa kutwaa taji la wachezaji wawili wawili kwa kushirikiana na dada yake, Venus Williams.

Katika mechi hiyo ya fainali iliyokuwa na ushindani mkali, Serena (30) na Venus (32) waliwabwaga Andrea Hlavackova na Lucie Hradecka wa Jamhuri ya Czech kwa 7-5, 6-4.

Taji alilotwaa Serena kwa wachezaji mmoja mmoja baada ya kumbwaga Radwanska lilikuwa la tano katika rekodi yake na la 14 katika michuano mbalimbali ya mchezo huo.

Safari hii Venus alishindwa kufika mbali katika michuano hiyo baada ya kutolewa raundi ya tano na Elena Vesnia wa Russia.

Venus na Serena waliwahi kutwaa taji la wachezaji wawili wawili katika michuano ya Wimbledon kuanzia mwaka 2000, 2002, 2008 na 2009

No comments:

Post a Comment