KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, July 8, 2012

Vladimir amdunda Thompson kwa KO



Bingwa wa dunia wa ndondi za uzani wa juu, Vladimir klitschko wa Russia juzi alifanikiwa kutetea taji lake baada ya kumdunda kwa knockout ya raundi ya sita, Tony Thompson wa Marekani.

Ushindi huo ulimwezesha Vladimir kuendelea kushikilia mataji yake yanayotambuliwa na WBA, IBF na WBO.

Thompson alilazimika kulamba sakafu katika dakika za mwisho za raundi ya tano baada ya kushindiliwa konde zito na Vladimir na hakuweza kuinuka.

Vladimir pia alimdondosha Thompson katika raundi ya sita na mwamuzi Sam Williams alimuhesabia kabla ya kuvunja pambano.

Hii ni mara ya pili kwa Vladimir kumdunda Thompson kwa knockout. Walipambana kwa mara ya kwanza mwaka 2008, ambapo Vladimir aliibuka mshindi kwa knockout ya raundi 11.

No comments:

Post a Comment