KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, July 15, 2012

MOROGORO YANG'ARA COPA COCA COLA

MOROGORO imetwaa ubingwa wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Copa Coca Cola baada ya kuifunga Mwanza bao 1-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Mshambuliaji Salum Ramadhani ndiye aliyefunga bao hilo la pekee dakika ya 36 baada ya kuunganisha wavuni pasi kutoka kwa Mtalemwa Katunzi.

Temeke ilifanikiwa kumaliza michuano hiyo ikiwa ya tatu baada ya kuichapa Tanga mabao 2-0.

Mabao yote ya Temeke yalifungwa na Rehani Kibingu dakika ya 48 na 86.

Kufuatia ushindi huo, Morogoro imezawadiwa sh. milioni nane wakati Mwanza imepata sh. milioni 4.4 na Temeke sh. milioni 3.2.

Tuzo ya kocha bora ilikwenda kwa kocha wa Tanga, Mohamed Kampira, tuzo ya mwamuzi bora imenyakuliwa na Liston Hiyari, kipa bora ni Shukuru Mohamed wa Temeke, mfungaji bora Mtelamwa Katunzi wa Morogoro na mchezaji bora ni Shiza Kichuya. Kila mmoja alipata sh 750,000. Tanga pia ilipata tuzo ya timu yenye nidhamu na kuzawadiwa sh. milioni moja.

No comments:

Post a Comment