KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, July 22, 2012

DROGBA AANZA RASMI KUICHEZEA SHANGHAI SHENHUA





Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba leo ameanza kuitumia rasmi klabu yake mpya ya Shanghai Shenhua baada ya kuiwezesha kutoka saye ya bao 1-1 dhidi ya Guangzhou.

Katika mechi hiyo ya ligi, Drogba aliingia uwanjani kipindi cha pili dhidi ya wapinzani wao, ambao walimaliza ligi kuu msimu uliopita wakiwa nafasi ya nne.

Drogba alitia saini mkataba wa kuichezea klabu hiyo kwa miaka miwili na nusu, akitokea klabu ya Chelsea ya England.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea ndiye aliyeiwezesha Shenhua kusawazisha baada ya kuwa nyuma kwa bao 1-0. Pasi ya Drogba ilimkuta Cao Yunding aliyeukwamisha mpira wavuni.

Wenyeji Guangzhou walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 22 kupitia kwa beki Moises wa Shenhua aliyejifunga wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira kwenye lango lake.

No comments:

Post a Comment