KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, July 10, 2012

YANGA YAITUNGUA JKT RUVU 2-0

TIMU ya soka ya Yanga jana iliichapa JKT Ruvu mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Yanga ikiwa chini ya kocha wake mpya, Tom Saintfiet kutoka Ubelgiji tangu alipoanza kuinoa wiki iliyopita.

Bao la kwanza la Yanga lilipachikwa wavuni na beki Nadir Haroub 'Cannavaro' dakika ya 18 kwa shuti baada ya mabeki wa JKT Ruvu kuzembea kuokoa mpira wa kona.

Hamisi Kiiza aliihakikishia Yanga ushindi dakika ya 72 baada ya kuifungia bao la pili, kufuatia pande safi alilomegewa na kiungo Haruna Niyonzima.

Katika mechi hiyo, beki Kelvin Yondan aling'ara kutokana na kucheza kwa uelewano mkubwa na Cannavaro, wakisaidiana na kiungo mkabaji, Athumani Iddi 'Chuji'.

No comments:

Post a Comment