Mabingwa watetezi Yanga leo wamefuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya soka ya Kombe la Kagame baada ya kuichapa Mafunzo ya Zanzibar kwa penalti 5-4. Katika mechi hiyo ya robo fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mshindi ilibidi apatikane kwa matuta baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya bao 1-1.
Katika kupigiana penalti, Yanga ilipata tano kupitia kwa Saidi Bahanuzi, Haruna Niyonzima, Nadir Haroub 'Cannavaro, Athumani Iddi na Hamisi Kiiza. Mafunzo ilipata tatu na kupoteza moja.
Licha ya kutolewa, Mafunzo ilionyesha kandanda safi na ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Walid Ibrahim kabla ya Bahanuzi kuisawazishia Yanga.
No comments:
Post a Comment