KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, July 1, 2012

Uwoya awafunika Wolper na Riyama

Irene Uwoya


Jacqueline Wolper


Riyama Ali



Aunty Ezekiel


MCHEZA filamu machachari Irene Uwoya ameibuka kidedea katika shindano la
kumsaka mcheza filamu bora wa kike lililoendeshwa na blogu ya liwazozito.
Katika shindano hilo lililoendeshwa kwa mwezi mmoja kwa wasomaji wa
blogu hiyo kuwapigia washiriki, Irene alipata kura 21, ambazo ni sawa na
asilimia 23.
Nafasi ya pili ilinyakuliwa na mwigizaji Jacqueline Wolper, aliyepata kura 17,
ambazo ni sawa na asilimia 19 wakati nafasi ya tatu ilichukulikuwa kwa
pamoja na Riyama Ali na Aunty Ezekiel, waliopata kura 15 kila mmoja,
ambazo ni sawa na asilimia 16.
Blandina Chagula , maarufu kwa jina la Johari alishika nafasi ya nne kwa
kupata kura 12, ambazo ni sawa na asilimia 13 wakati Rose Ndauka alishika
nafasi ya tano kwa kupata kura tisa, ambazo ni sawa na asilimia 9.
Mwanadada Jacque Pentzel ndiye pekee, ambaye hakupata kura katika
shindano hilo licha ya kuwa ni mmoja wa waigizaji wazuri wa Kibongo.
Blogu ya liwazozito inawashukuru wasomaji wake wote walioshiriki kuwapigia
kura wacheza filamu hao, ikiamini kwamba walipiga kura hizo kwa kuzingatia
uwezo na mvuto wao katika fani hiyo.

No comments:

Post a Comment