KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, May 30, 2013

TAIFA STARS YAIPA MCHECHETO SUDAN



MAZOEZI makali yanayofanywa na kikosi cha timu ya soka ya Taifa, 'Taifa Stars' nchini Ethiopia kimeifanya timu ya Taifa ya Sudan kuanza kuingiwa na hofu.

Taifa Stars inatarajiwa kumenyana na Sudan mwishoni mwa wiki hii katika mchezo wa kirafiki wa kimatifa utakaofanyika katika Uwanja wa Addis Ababa, Ethiopia.

Meneja wa Taifa Stars, Leopod Tasso Mukebezi alisema kwa njia ya simu jana kutoka Ethiopia kuwa, timu hiyo iliwasili nchini humo juzi na kuweka kambi katika hoteli ya Hilton kabla ya kuanza mazoezi jana asubuhi.

Tasso alisema baada ya Taifa Stars kuanza mazoezi, maofisa wa benchi la ufundi la Sudan walifika uwanjani kwa lengo la kufuatilia mazoezi hayo.

Meneja huyo alisema ujio wa Wasudan nchini Ethiopia umeonyesha wazi kuwa, wameingiwa na wasiwasi kuhusu mechi hiyo, ambayo ni sehemu ya maandalizi kwa Taifa Stars kabla ya kumenyana na Morocco.

Tasso alisema kambi ya timu hiyo inaendelea vizuri na wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakiwa na hamu kubwa ya kuvaana na Morocco.

Taifa Stars inatarajiwa kumenyana na Morocco, Juni 8 mwaka huu mjini Marrakech katika mchezo wa marudiano wa kundi C wa michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia za 2014.

Wachezaji wa Taifa Stars waliokwenda Ethiopia ni nahodha Juma Kaseja, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir na Mwinyi Kazimoto.

Wengine ni Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

No comments:

Post a Comment