'
Friday, May 24, 2013
KOCHA WA AZAM AKATAA OFA KUTOKA LIBYA NA CANADA
KOCHA Mkuu wa Azam, Stewart Hall amesema amekataa ofa ya mamilioni ya fedha kutoka katika klabu mbalimbali za soka za Libya na Canada zilizokuwa zinamtaka.
Stewart aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana kuwa, alipokea ofa hizo muda mfupi baada ya kumalizika kwa michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara.
Kocha huyo kutoka Uingereza alisema, ameshindwa kuzikubali ofa hizo kwa sababu bado anataka kuendelea kuinoa Azam kwa muda mrefu ili aweze kutimiza malengo yake.
Stewart alisema viongozi wa Azam wamemtaka aendelee kuinoa timu hiyo kwa msimu mmoja zaidi.
"Hakuna kocha anayekataa ofa ya mamilioni ya fedha, lakini kitu kikubwa ninachoangalia kwa sasa ni uhuru na mazingira ya kazi,"alisema.
Stewart alianza kuinoa Azam, 2011na kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi na nafasi ya pili katika Kombe la Kagame kabla ya kutimuliwa na kujiunga na Sofapaka ya Kenya.
Alirejea nchini Desemba mwaka jana na kuendelea kuinoa Azam, ambayo ilifuzu kucheza raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho na kushika nafasi ya pili katika ligi kuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment