KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 3, 2012

Taifa Stars yachapwa 2-0 na Ivory Coast

Mshambuliaji Didier Drogba wa Ivory Coast akijiandaa kutuliza mpira huku akiwa amezongwa na beki Kevin Yondan wa Taifa Stars.

Mshambuliaji Mbwana Samatta wa Taifa Stars akiruka hewani kupiga mpira kwa kichwa sambamba na beki wa Ivory Coast.

Moja ya kosa kosa zilizotokea kwenye lango la Ivory Coast wakati timu hiyo ilipomenyana na Taifa Stars jana.

Shaaban Nditi (kushoto) wa Taifa Stars akijaribu kumshibiti Solomon Kalou wa Ivory Coast.

TIMU ya soka ya Taifa,Taifa Stars jana ilipigwa mweleka wa mabao 2-0 na Ivory Coast katika mechi ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia za 2014.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan, Ivory Coast ilijipatia mabao hayo mawili, moja katika kila kipindi.

Bao la kwanza lilifungwa na Salomon Kalou katika kipindi cha kwanza kabla ya Didier Drogba kuongeza la pili katika kipindi cha pili.

Taifa Stars ililazimika kumaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 baada ya beki wake, Aggrey Morris kutolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Slim Jedidi kutoka Tunisia kwa kosa la kucheza rafu mbaya.

Katika mechi hiyo, Kocha Kim Poulsen wa Taifa Stars alilazimika kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili kutoka katika kikosi alichokichezesha katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Malawi iliyochezwa Mei 26 mwaka huu.

Kim aliamua kumchezesha Amir Maftah katika nafasi ya beki wa kushoto badala ya Waziri Salum na pia alimchezesha Mrisho Ngasa katika nafasi ya mshambuliaji wa kati badala ya Haruna Moshi, ambaye hakwenda Ivory Coast kutokana na kuwa majeruhi.

No comments:

Post a Comment