KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, October 22, 2013

UCHAGUZI MKUU BODI YA LIGI IJUMAA



Uchaguzi wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPL Board) utafanyika Oktoba 25 mwaka huu
kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Golden Jubilee Tower.

Kwa mujibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
wajumbe wanaounda Mkutano wa Uchaguzi ni wenyeviti kutoka klabu 24 za Ligi
Daraja la Kwanza (FDL), na 14 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Wagombea kwenye uchaguzi huo ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Said
Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti) wakati wanaoumba ujumbe wa
Kamati ya Uendeshaji ni Khatib Omari Mwindadi na Kazimoto Muzo.

No comments:

Post a Comment