KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, October 10, 2013

WEMA: ACHENI KUNIONEA, NIMEWAKOSEA NINI?


BAADA ya ukimya wa muda mrefu, mcheza filamu machachari, Wema Sepetu ameibuka na kuvitaka vyombo vya habari viache kumfuatafuata na kuchafua jina lake.

Wema amesema haelewi ni kwa nini vyombo vya habari vimekuwa vikimchafua mara kwa mara na ameiita tabia hiyo kuwa ni ya kionevu na iliyolenga kumkatisha tamaa kimaisha.

"Mara ya mwisho nililia wakati nilipoambiwa nina pepo la ngono. Leo hii nalia tena baada ya kuambiwa nimekamatwa na unga (dawa za kulevya) China na nitanyongwa," ameeleza Wema wiki hii kupitia akaunti yake ya mtandao wa intergram.

Wema ameamua kutoa dukuduku lake hilo, kufuatia taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini hivi karibuni kwamba, amekamtwa na dawa za kulevya China na amehukumiwa kunyongwa.

"Siwezi kusema kwamba nina furaha, sina furaha kabisa na sikuwahi kufikiria kwamba magazeti yetu, ipo siku yatakuwa na nguvu ya kuandika uongo wa namna hii," ameeleza Wema kupitia mtandao huo.

"Kwa sababu huwa nakaa kimya, ndio muone kwamba mnaweza kunionea muda wote! Roho inaniuma sana. Naumia kwa sababu nimechoka kuchafuliwa jina langu bila sababu za msingi.

"Nimesema nitoke zangu kimya kimya kuja huku (China), kujihangaikia zangu kuhusu kazi zangu, lakini nimeonekana nimekuja kuuza unga na nitanyongwa hivi karibuni.

"Ni lini nyinyi watu mtaniacha niishi kwa amani? Sidhani kama nilishawahi kumkosea yeyote kati yenu.

"Maskini ya Mungu naishi maisha yangu mwenyewe, sina habari na mtu, sijawahi hata kufikiria kufanya upuuzi huo, nimeumia sana. Mungu nisaidie," amesema Wema kupitia akaunti yake hiyo.

No comments:

Post a Comment