KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, October 3, 2013

MOTO WATEKETEZA MALI ZA NIYONZIMA



Haruna Niyonzima akiwa amekaa nyumbani kwake Magomeni baada ya kumaliza kuzima shoti ya umeme iliyokuwa inateketeza mali zake

Kiungo wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima, ambaye pia ni mchezaji wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, Young Africans amepatwa na janga la kuunguliwa kwa baadhi ya mali zake, kufuatia kutokea shoti ya umeme leo asubuhi.

Niyonzima, ambaye anaishi eneo la Magomeni Makuti, Dar es Salaam, amekutwa na tatizo hilo leo saa 12 asubuhi, akiwa anajiandaa kwenda mazoezini.

Mchezaji huyo alishtuka kuona moshi ukifuka kutokea eneo la sebuleni kwake na aliposogea, alibani ni moto ulikuwa ukiwaka.

"Nilisikia hewa nzito ndani, nikaamka kuelekea sebuleni, nilipofika nilikuta moto umetanda chumba kizima, ndipo majirani walijitokeza na kuanza kutusaidia kuzima moto huo kwa kuvunja madirisha ya vioo na kumwaga maji ili moto huo uzimike," alisema Niyonzima

"Nashukuru tulifanikiwa kuuzima moto baada ya muda kwa kushirikiana na majirani, lakini vitu vyote vilivyokuwa ndani hatukufanikiwa kuivitoa vikiwa salama. Baadhi ya vitu vilivyoungua ni pamoja na luninga iliyokua imefungwa ukutani, redio (music system), makochi na fenicha za ndani,"aliongeza.

Niyonzima alisema anahisi moto huo ulitokana na shoti ya umeme juu ya dari kwa vile ndio sehemu iliyokuwa chanzo cha moto huo.

Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alifika nyumbani kwa Niyonzima saa mbili
asubuhi na kuzungumza na mchezaji huyo, ambaye alisema anashukuru familia yake iko salama na hakuna aliyedhurika zaidi ya vitu vilivyoteketea na moto.

Uongozi wa Yanga umempa pole Niyonzima kwa matatizo yaliyomfika na kumuomba Mungu amjalie nguvu na uvumilivu na kwamba upo pamoja naye katika wakati huu mgumu.

No comments:

Post a Comment