KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, October 28, 2013

AZAM YAISHUSHA SIMBA KILELENI


AZAM jioni ya leo imeukwaa uongozi wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Simba mabao 2-1 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo umeiwezesha Azam kuwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 10 wakati Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 20.

Hata hivyo, Azam inaweza kuenguliwa kileleni mwa ligi hiyo iwapo Mbeya City itawabwaga ndugu zao wa Prisons kesho katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mabingwa watetezi Yanga wanaweza kuchupa nafasi ya pili iwapo kesho wataifunga Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Taifa.

Kwa sasa, Yanga inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 10 na iwapo itashinda kesho, itafikisha pointi 22.

Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Ramadhani Singano 'Messi' kabla ya John Bocco kuisawazishia Azam na Kipre Tchetche kuongeza la pili.

No comments:

Post a Comment