'
Thursday, October 3, 2013
MABAO 90 YAFUNGWA LIGI KUU
JUMLA ya mabao 90 yameshatinga wavuni hadi sasa katika michuano ya soka ya ligi kuu ya Tanzania Bara, inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Katika mabao hayo, Simba inaongoza kwa kufunga mabao 15, ikifuatiwa na Yanga iliyofunga mabao 11 na Azam iliyofunga mabao tisa. Kagera Sugar na Rhino Rangers zinashika nafasi ya nne kwa kufunga mabao saba kila moja.
Coastal Union, JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Mbeya City zinashika nafasi ya tano kwa kufunga mabao sita kila moja, zikifuatiwa na Mtibwa Sugar iliyofunga mabao matano na Ashanti yenye mabao manne. JKT Oljoro na Prisons zimefunga mabao matatu kila moja wakati Mgambo JKT imeambulia mabao mawili.
Ashanti ndiyo timu yenye ngome dhaifu kuliko zote hadi sasa baada ya kuruhusu kufungwa mabao 15, ikifuatiwa na Mgambo JKT iliyofungwa mabao 10 na Prisons iliyochapwa mabao tisa.
Rhino Rangers imefungwa mabao manane, ikifuatiwa na Yanga iliyofungwa mabao saba, Mtibwa Sugar, JKT Oljoro na Azam zimefungwa mabao sita kila moja, Mbeya City imefungwa mabao matano wakati Ruvu Shooting, JKT Ruvu na Simba zimefungwa mabao manne kila moja.
Kagera Sugar na Coastal Union ndizo zenye ngome ngumu kuliko timu zote kutokana na kufungwa mabao matatu kila moja.
Timu pekee, ambazo hazijaonja ladha ya ushindi katika ligi hiyo hadi sasa ni Prisons na Ashanti wakati Simba inaongoza kwa kushinda mechi nne kati ya sita, ikifuatiwa na Kagera Sugar, JKT Ruvu na Ruvu Shooting zilizoshinda mechi tatu kila moja.
Timu zilizoambulia ushindi katika mechi mbili ni Azam, Coastal Union na Yanga wakati timu zilizoambulia ushindi wa mechi moja ni Mbeya City, Rhino Rangers, Mtibwa Sugar, JKT Oljoro na Mgambo JKT.
Simba inaongoza ligi hiyo kwa kuwa na pointi 14 baada ya kucheza mechi sita, ikifuatiwa na Kagera Sugar yenye pointi 11 wakati Azam na Coastal Union zinashika nafasi ya tatu na nne, zikiwa na pointi 10 kila moja.
Mabingwa watetezi Yanga wanashika nafasi ya tano kwa kuwa na pointi tisa, sawa na JKT Ruvu na Ruvu Shooting, Mbeya City ni ya nane ikiwa na pointi nane, Rhino na Mtibwa zinashika nafasi ya tisa na kumi zikiwa na pointi saba kila moja wakati JKT Oljoro na Mgambo JKT zinashika nafasi ya 11 na 12 zikiwa na pointi tano kila moja.
Prisons ni ya 13 ikiwa na pointi nne wakati Ashanti inashika mkia kwa kuwa na pointi mbili.
Wakati huo huo, mshambuliaji Hamisi Tambwe anaongoza kwa ufungaji mabao katika ligi kuu ya Tanzania Bara.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Burundi amefunga mabao saba katika mechi tano alizoichezea Simba hadi sasa. Tambwe hakucheza mechi ya kwanza dhidi ya Rhino Rangers kutokana na kukosa hati ya uhamisho wa kimataifa.
Tambwe hadi sasa anashikilia rekodi ya kufunga mabao manne katika mechi moja baada ya kuifungia Simba idadi hiyo ya mabao ilipoibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Mgambo JKT.
Mrundi huyo pia aliifungia Simba mabao mawili ilipotoka sare ya mabao 2-2 na Mbeya City kabla ya kufunga bao lingine mwishoni mwa wiki iliyopita katika mechi dhidi ya JKT Ruvu, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Tambwe anafuatiwa kwa karibu na Jerry Tegete , Didier Kavumbagu (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Kipre Tchetche (Azam) na Peter Michael (Prisons) waliofunga mabao matatu kila mmoja.
Waliofunga mabao mawili kila mmoja ni Jonas Mkude (Simba), Jerry Santo, Haruna Moshi (Coastal Union), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Elias Maguri (Ruvu Shooting), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Paul Nonga, Mwagani Yeya (Mbeya City), Hamis Kiiza (Yanga), Themi Felix (Kagera Sugar) na Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar).
RATIBA YA MECHI ZIJAZO ZA LIGI HIYO NI KAMA IFUATAVYO:
Jumamosi, 5,2013
Ruvu Shjooting vs Simba
JKT Ruvu vs Kagera Sugar
Coastal Union vs Azam
JKT Oljoro vs Mbeya City
Jumapili; 6, 2013
Mgambo JKT vs Prisons
Yanga vs Mtibwa Sugar
Oktoba 9, 2013
Rhino Rangers vs Mbeya City
JKT Oljoro vs Ruvu Shooting
Azam vs Mgambo JKT
Mtibwa vs JKT Ruvu
Oktoba12, 2013
Kagera Sugar vs Yanga
Simba vs Prisons
Oktoba 13, 2013
Ashanti vs Coastal Union
MSIMAMO WA LIGI HIYO HADI SASA NI KAMA IFUATAVYO:
P W D L GF GA PTS
1 Simba SC 6 4 2 0 15 4 14
2 Kagera Sugar 6 3 2 1 7 3 11
3 Azam 6 2 4 0 9 6 10
4 Coastal Union 6 2 4 0 6 3 10
5 Yanga 6 2 3 1 11 7 9
6 JKT Ruvu 6 3 0 3 6 4 9
6 Ruvu Shooting 6 3 0 3 6 4 9
8 Mbeya City 6 1 5 0 6 5 8
9 Rhino Rangers 7 1 4 2 7 8 7
10 Mtibwa Sugar 6 1 4 1 5 6 7
11 JKT Oljoro 6 1 2 3 3 6 5
12 Mgambo JKT 6 1 2 3 2 10 5
13 Prisons 6 0 4 2 3 9 4
14 Ashanti United 7 0 2 5 4 15 2
WAFUNGAJI MABAO
7- Hamisi Tambwe (Simba)
3- Jerry Tegete , Didier Kavumbagu (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Kipre Tchetche (Azam), Peter Michael (Prisons).
2- Jonas Mkude (Simba), Jerry Santo, Haruna Moshi (Coastal Union), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Elias Maguri (Ruvu Shooting), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Paul Nonga, Mwagani Yeya (Mbeya City), Hamis Kiiza (Yanga), Themi Felix (Kagera Sugar), Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar).
1- Abdi Banda, Crispian Odulla,(Coastal Union), Henry Joseph, Betram Mombeki, Ramadhani Singano (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Khamis Mcha, Aggrey Morris, John Bocco, Joseph Kimwaga (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader (Ruvu Shooting), Juma Luzio, Masoud Ally, Shaaban Nditti, (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Tumba Swedi, Paul Maono (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Salum Machaku, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Godfrey Wambura, Clement Douglas (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary, Paul Malipesa (Oljoro JKT)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment