KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, October 22, 2013

SIMBA, YANGA DIMBANI TENA KESHO


Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Oktoba 23 mwaka huu) kwa mechi tatu; ambapo Yanga itaikaribisha Rhino Rangers katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Coastal Union inaikaribisha Simba katika mechi itakayopigwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga na kuchezeshwa na mwamuzi Dominic Nyamisana kutoka Dodoma.

Tanzania Prisons ambayo imepoteza mechi mbili zilizopita ugenini dhidi ya Ashanti United na Simba inarejea uwanja wake wa Kumbukumbu ya Sokoine kwa kuikaribisha Kagera Sugar.

Nayo Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea kesho (Oktoba 23 mwaka huu) kwa mechi moja ya kundi A itakayozikutanisha Tessema na Villa Squad kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.


RAMBIRAMBI MSIBA WA JIMMY MHANGO
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo
cha mjumbe wa Bodi ya klabu ya Ashanti United, Jimmy Mhango kilichotokea jana
(Oktoba 21 mwaka huu).

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani Mhango aliutumikia
mpira wa miguu kwa muda mrefu, tangu akiwa mchezaji, kocha na baadaye
kiongozi.

Kabla ya kuingia kwenye Bodi ya Ashanti United, enzi za uchezaji wake alichezea
timu za Mapinduzi ya Dodoma, Ushirika ya Moshi na Pan African ya Dar es Salaam.
Pia aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa Ashanti United.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Mhango, klabu ya Ashanti United na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), na kuwataka kuwa na
subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Maziko yamefanyika leo mchana katika makaburi ya Abeid (Mchikichini) Dar es
Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Mhango mahali pema peponi. Amina

No comments:

Post a Comment