KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, October 24, 2013

WEMA: SIMFIKIRII DIAMOND, NAWAZA PESA



HATIMAYE mcheza filamu machachari, Wema Sepetu ameamua kuvunja ukimya kwa kusema, kamwe hamfikirii mpenzi wake wa zamani, Naseeb Abdul 'Diamond' katika akili yake.

Wema amesema siku zote kitu cha kwanza kinachomuijia akilini ni jinsi ya kutafuta pesa na kuzitumia.

"Watu wengi, hasa vyombo vya habari, vimekuwa vikidhani akili yangu siku zote ipo kwa Diamond, kwamba siku zote namuwaza Diamond," ameandika binti huyo kwenye mtandao wa twitter wiki hii.

"Diamond hayupo kwenye kichwa cha Wema, muda wote nafikiria pesa," amesisitiza  mrembo huyo wa zamani wa Tanzania.

Kauli hiyo ya Wema imekuja siku chache baada ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini, kuchapisha picha alizopiga pamoja na Diamond walipokutana hivi karibuni barani Asia hivi karibuni.

Picha hizo zilikwenda sambamba na maelezo kuhusu Wema na Diamond, kwamba bado wapo kwenye mapenzi mazito, licha ya Diamond kutangaza kuwa wameachana na sasa yuko na mpenzi wake mpya, anayejulikana kwa jina la Penny.

Katika maelezo aliyoyatoa kwenye mtandao wa twitter, Wema ameweka picha zake mbili, moja ikiwa na picha ndogo ya Diamond pembeni yake, ikiwa na maneno yanayosema: ' Wanachofikiria namuwaza Diamond'.

Katika picha nyingine, Wema ameweka picha ndogo inayoonyesha maburungutu ya noti za dola za Marekani, ikiwa na maneno yanayosema: 'Ninachokifiria ni pesa'.

Wema ameelezea msimamo wake huo siku chache baada ya kuvitaka vyombo vya habari viache kumfuatafuata na kuchafua jina lake.

Mwanadada huyo alisema haelewi ni kwa nini vyombo vya habari vimekuwa vikimchafua mara kwa mara na ameiita tabia hiyo kuwa ni ya kionevu na iliyolenga kumkatisha tamaa ya maisha.

"Mara ya mwisho nililia wakati nilipoambiwa nina pepo la ngono. Leo hii nalia tena baada ya kuambiwa nimekamatwa na unga (dawa za kulevya) China na nitanyongwa," alieleza Wema kupitia akaunti yake ya mtandao wa intergram.

Wema aliamua kutoa dukuduku hilo, kufuatia taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini hivi karibuni kwamba, amekamtwa na dawa za kulevya China na amehukumiwa kunyongwa.

"Siwezi kusema kwamba nina furaha, sina furaha kabisa na sikuwahi kufikiria kwamba magazeti yetu, ipo siku yatakuwa na nguvu ya kuandika uongo wa namna hii," alieleza Wema kupitia mtandao huo.

"Kwa sababu huwa nakaa kimya, ndio muone kwamba mnaweza kunionea muda wote! Roho inaniuma sana. Naumia kwa sababu nimechoka kuchafuliwa jina langu bila sababu za msingi.

"Nimesema nitoke zangu kimya kimya kuja huku (China), kujihangaikia zangu kuhusu kazi zangu, lakini nimeonekana nimekuja kuuza unga na nitanyongwa hivi karibuni. Ni lini nyinyi watu mtaniacha niishi kwa amani? Sidhani kama nilishawahi kumkosea yeyote kati yenu.

"Maskini ya Mungu naishi maisha yangu mwenyewe, sina habari na mtu, sijawahi hata kufikiria kufanya upuuzi huo, nimeumia sana. Mungu nisaidie," alieleza Wema kupitia akaunti yake hiyo.

No comments:

Post a Comment