KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, October 10, 2013

SAGNA AMPASUA KICHWA WENGER



LONDON, England
KLABU ya Arsenal ya England, imeanza kufanya mipango ya kumbakiza beki wake nyota, Bacary Sagna, ambaye ameweka bayana kuwa anataka kuondoka Emirates.

Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, unamalizika mwishoni mwa msim huu na Arsenal imeingiwa na hofu kuwa anaweza kuondoka akiwa huru.

Arsenal imeshafungua milango kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya na mchezaji huyo, lakini Sagna ameonekana kuweka ngumu baada ya msimu uliopita kulalamika akidai maboresho ya mkataba wake.

Sagna, anapewa nafasi kubwa ya kuihama Arsenal wakati wa usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao, lakini kocha Mfaransa Arsene Wenger, amekuwa akihaha kutaka kumbakiza.

Kinachomfanya Wenger ahahe kumbakiza beki huyo, ni uhodari wake wa kuwazuia washambuliaji wa timu pinzani na kupanda mbele kusaidia mashambulizi.

Sagna analipwa mshahara wa pauni 60,000 (sh. milioni 125) kwa wiki, na amekuwa akihusishwa na mipango ya kurejea Ufaransa kujiunga na klabu za Paris Saint Germain (PSG) au Monaco.

Beki huyo aliwahi kuzitosa Real Madrid na Manchester City, zilizokuwa zikimuwania kwa misimu tofauti baada ya kuahidiwa maboresho ya mkataba wake.

Mchezaji huyo alijiunga na Arsenal  2008, baada ya kumvutia Wenger alipokuwa akichezea klabu ya Marseille.

Tayari klabu kongwe zinazocheza Ligi Kuu ya Uturuki, Galatasary na Fenerbache, zimeonyesha nia ya kumsajili beki huyo wakati usajili wa dirisha dogo Januari, mwakani.

No comments:

Post a Comment