KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, October 22, 2013

KIINGILIO MECHI YA TWIGA STARS NA MSUMBIJI BUKU


Kiingilio cha chini kwenye mechi ya wanawake chini ya miaka 20 katika ya Tanzania
na Msumbiji itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 1,000.

Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni, na kiingilio hicho ni kwa ajili ya viti
vya rangi ya kijani, bluu na chungwa. Viingilio vingine ni sh. 2,000 kwa VIP C, sh.
5,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 10,000.

Timu ya Msumbiji inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Oktoba 23 mwaka huu) saa 8
kamili mchana kwa ndege ya LAM. Msumbiji yenye msafara wa watu 25 itafikia
kwenye hoteli ya Sapphire.

SERENGETI BOYS YAALIKWA MICHUANO YA ANOCA
Timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Serengeti
Boys) imealikwa kushiriki Olimpiki ya Afrika itakayofanyika Mei mwakani.

Mpira wa miguu ni kati ya michezo 22 itakayoshindaniwa katika mashindano
yatakayofanyika Gaborone, Botswana chini ya Kamati za Olimpiki za Afrika
(ANOCA).

Kwa mujibu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC), Tanzania imepewa nafasi ya
kushiriki katika michezo hiyo ya Olimpiki kwa Afrika kutokana na kuwa na programu
nzuri za vijana hasa chini ya umri wa miaka 17.

Hiyo itakuwa ni michezo ya Pili ya Afrika kwa Olimpiki ambapo ya Kwanza ilifanyika
mwaka 2010 jijini Rabat, Morocco.

No comments:

Post a Comment