KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, October 26, 2013

MABINTI WA KIBONGO WAWAFANYIA MAUAJI WENZAO WA MSUMBIJI





Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam

TIMU ya soka ya taifa ya wanawake kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, The Tanzanites imeifunga Msumbiji mabao 10-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia kwa mabinti wa umri huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.

Katika mchezo huo uliohudhuria na mashabiki wachache mno, hadi mapumziko, tayari Tanzanites walikuwa mbele kwa mabao 5-0

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya sita na Neema Paul aliyeunganisha pasi ya Theresa Yona, kutoka wingi ya kushoto, wakati mfungaji bora wa michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika mwaka huu Nigeria, Shelder Boniface alifunga la pili dakika ya 24 baada ya kupangua ngome na kumpiga chenga hadi kipa.

Deonesia Daniel akafunga bao la tatu kwa shuti kali la mpira wa adhabu lililotinga moja kwa moja nyavuni dakika ya 32 na dakika ya 41, Amina Ali akafunga la nne kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la mita 18

Shelider Boniface alifunga bao ambalo lingekuwa la tano dakika ya 45, lakini refa Ines Niyonsara wa Burundi akakataa.

Kipindi cha pili The Tanzanites inayofundishwa na Rogasian Kaijage ilirudi na moto wake na kufanikiwa kupata bao tano, mfungaji Neema Paul aliyeunganisha krosi ya Theresa Yona.

Hatimaye Shelder alifunga bao la sita dakika ya 80 akimalizia mpira uliotemwa na kipa kufuatia shuti la Stumai Abdallah.

Dakika ya 82 Tanzania ikapata bao saba kupitia kwa Amina Ali aliyefumua shuti kutoka katikati ya Uwanja.

Tanzanites walipata bao la nane dakika ya 86 kupitia kwa Deonesia Daniel aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, baada ya Shelder Boniface kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Dakika ya 89 Tanzania ilipata bao tisa kupitia kwa Amina Ali tena, ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo. Stumai Abdallah akaifungia Tanzania bao la 10 dakika ya 90.

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Celina Julius, Stumai Abdallah, Maimuna Said/Amina Hebron dk60, Fatuma Issa, Anastazia Anthony, Deonisia Daniel, Vumilia Maarifa, Amina Ali, Neema Paul, Shlder Boniface na Theresa Yona.

Msumbiji; Paulina Jambo/Catarina Francue dk50, Esperanca Malaita/Delice Assane dk52, Felismisa Moiane, Emma Paulino, Gilda Macamo, Deolinda Gove, Jessica Zunguene, Cidalia Cuta, Nelia Magate, LonicaTsanwane na Onesema David.

IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA BINZUBEIRY

No comments:

Post a Comment