KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, May 14, 2010

Makocha wa Ilala, Temeke watambiana

MAKOCHA wa timu za mikoa ya Ilala na Temeke wametamba kuwa, watahakikisha timu zao zinafuzu kucheza fainali ya michuano ya Kombe la Taifa mwaka huu.

Makocha hao, Jamhuri Kihwelo wa Ilala na Habibu Kondo wa Temeke walitoa majigambo hayo Jumatano iliyopita mara baada ya timu zao kufuzu kucheza robo fainali ya michuano hiyo.

Ilala ilitinga robo fainali baada ya kushinda mechi zake mbili dhidi ya Mtwara na Lindi na kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Ruvuma katika mechi ya mwisho. Ilala ilipangwa kituo cha Mtwara.

“Tunamshukuru Mungu kwamba tumefuzu kucheza robo fainali, kilichobaki sasa ni kuhakikisha tunatoa kichapo kwa kila timu tutakayokutana nayo na kutwaa ubingwa,”alijigamba Kihwelo.

Aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kujituma na kuiwezesha timu hiyo kusonga mbele, licha ya kupata upinzani mkali kutoka kwa timu walizocheza nazo.

Kihwelo aliiwezesha Ilala kutwaa kombe hilo mara mbili mfululizo na mwaka huu inashiriki tema mashindano hayo kama bingwa mtetezi.

Naye Kondo alisema baada ya kutinga robo fainali, haoni kipi kitakachoikwamisha timu yake kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Beki huyo wa zamani wa timu ya Sigara alisema, wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kwenye mechi za hatua ya makundi kutokana na timu yake kutofanya maandalizi mazuri.

"Hatuiogopi timu yoyote tutakayopangwa nayo katika robo fainali, yoyote atakayekuja mbele yetu, tutahakikisha tunamchinja na kusonga mbele hadi fainali,”alisema.

No comments:

Post a Comment