KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, March 10, 2013

YANGA HAIKAMATIKI, YAITUNGUA TOTO AFRICAN 1-0




YANGA jana iliendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya soka ya ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Toto African bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo uliiwezesha Yanga kujikita zaidi kileleni mwa ligi hiyo, ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 19, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 37.

Toto African ililianza pambano hilo kwa kasi na kufanya mashambulizi makali kwenye lango la Yanga, lakini wachezaji wake, Mussa Mussa, Mohamed Jingo na Chika Oluge walishindwa kuzitumia vyema nafasi walizopata kufunga mabao. Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa suluhu.

Yanga ilizinduka dakika ya 48 na 53 wakati Hamisi Kiiza na Jerry Tegete walipoingia na mpira ndani ya 18, lakini mashuti yao hayakuweza kulenga lango.

Toto African ilipata pigo dakika ya 68 baada ya mchezaji wake Eric Mlilo kutolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Andrew Shamba kutoka Pwani kwa kosa la kucheza rafu mbaya.

Bao pekee na la ushindi la Yanga lilifungwa na Nizar Khalfan dakika ya 70. Alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi kutoka kwa Kiiza.

No comments:

Post a Comment