KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, March 7, 2013

SIMBA YAMEGUKA VIPANDE



KLABU ya Simba inaelekea kumeguka vipande vipande baada ya makamu mwenyekiti, Godfrey Nyange 'Kaburu' na mjumbe wa kamati ya utendaji na mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hanspope kutangaza kujiuzulu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kaburu alisema amemuandikia barua Rage kumfahamisha kuhusu uamuzi wake huo.

Hata hivyo, Rage hakuweza kupatikana jana baada ya kuwepo na taarifa kwamba, amekwenda India kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya mgongo.

Kaburu amekuwa kiongozi wa pili wa kamati ya utendaji ya Simba kutangaza kujiuzulu leo. Mapema asubuhi, Hanspope alitangaza kujiuzulu nyadhifa zote mbili kwa kile alichodai kutoridhishwa na mwenendo wa ndani ya klabu hiyo.

Hanspope alisema pia kuwa, licha ya kuwa kwenye uongozi wa Simba kwa zaidi ya miakia mitatu na kujitolea pesa zake, haoni mafanikio yoyote aliyoyatarajia.

No comments:

Post a Comment