KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, March 10, 2013

SIMBA YAWAFUTA MACHOZI MASHABIKI WAKE




SIMBA jana iliwafuta machozi mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kutokana na ushindi huo, Simba sasa imefikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 19, ikiwa nyuma ya Yanga yenye pointi 45 na Azam yenye pointi 37.

Katika mechi hiyo, Kocha Patrick Liewig wa Simba aliamua kuwapumzisha wachezaji wake nyota kadhaa na kuamua kuwachezesha chipukizi.

Baadhi ya wachezaji nguli waliowekwa benchi katika mechi hiyo ni Juma Kaseja, Haruna Moshi, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Juma Nyoso na Amir Maftah.

Wachezaji chipukizi waliocheza mechi hiyo ni mabeki Miraji Adamu na Hassan Khatib, viungo Jonas Mkude, Rashid Ismail , Abdalla Seseme, Ramadhani Singano na Chanongo.

Iliwachukua Simba dakika 34 kuhesabu bao la kwanza lililofungwa na Mrisho Ngasa kabla ya kuongeza la pili dakika ya 44 lililofungwa na Haruna Chanongo.

Bao la kujifariji la Coastal Union lilifungwa na kiungo Razak Khalfan dakika ya 49 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Ibrahim Twaha.



No comments:

Post a Comment