KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, March 4, 2013

SIMBA AIBU TUPU, AZAM YAMEREMETA




WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa Afrika, Simba jana walitolewa raundi ya kwanza baada ya kuchapwa mabao 4-0 na Recreativo Libolo ya Angola katika mechi ya marudiano iliyochezwa mjini Caluco.

Kipigo hicho kiliifanya Simba itolewe kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-0 baada ya kuchapwa bao 1-0 katika mechi ya awali iliyochezwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ilikuwa ikihitaji ushindi wa mabao 2-0 ili iweze kusonga mbele, lakuini kutokana na kiwango duni ilichoonyesha katika mchezo huo, uwezekano wa kupata ushindi ulikuwa finyu.

Wakati Simba ikiangukia pua, wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Azam walisonga mbele kwa kishindo baada ya kuibugiza Al Nasir ya Juba mabao 4-0.

Katika mechi hiyo iliyokuwa ya upande mmoja, iliyochezwa mjini Juba, mshambuliaji John Bocco aliifungia Azam mabao mawili.

Mabao mengine ya Azam yalifungwa na Khamis Mcha na Kipre Tchetche.

Kutokana na ushindi huo, Azam imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1.

No comments:

Post a Comment