KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, March 12, 2013

SIPHO MAKHABANE KUTUMBUIZA TAMASHA LA PASAKA DAR



BAADA ya mwaka jana mwimbaji mahiri Rebecca Malope wa Afrika Kusini kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka jijini Dar es Salaam, mwaka huu ni zamu yam kali mwingine kutoka nchini humo Sipho Makhabane.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, ilieleza kuwa raia huyo wa Afrika Kusini amethibitisha atakuja kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Ni mafanikio mengine kwa tamasha la mwaka huu, mwaka jana tulifanikiwa kumpata Malope, mwaka huu tumepiga hatua nyingine ya kumleta Sipho,” ilisema taarifa ya lisema Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Msama.

Kuthibitisha kushiriki tamasha hilo kwa msanii huyo kunafanya idadi ya wasanii kutoka nje ya Tanzania watakaokuja kutumbuiza hadi sasa kufikia wane.

Wasanii wengine wa nje ya Tanzania ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hili ni , Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda inayotamba na albamu ya Mtegemee Yesu. Wasanii wa Tanzania waliothibitisha hadi sasa ni Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu.

“Ni msanii mwenye uwezo mkubwa na aliyejijengea jina, hivyo ujio wake ni jambo la kufurahia,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa msanii huyo amekuwa akipata mafanikio katika muziki wa Injili karibu kila mwaka.

Baadhi ya nyimbo zake ni Moya Wami, Indonga, Akukhalwa, Over&Over, Nguy’zolo, Yizwa Nkosiseju, Hlalanami Nkosi Jesu, Yek’intokozo, Injabulo, Hlalanami Jesu, Makadunyiswe, Vuka Mphemlo, Mphefumlo na Moya Wami.

Wasanii wa Tanzania ambao watashiriki tamasha hilo mwaka huu ni Rose Muhando, John Lissu, Upendo Nkone, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

No comments:

Post a Comment