KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, March 6, 2013

KILINDA KUBWAGA MANYANGA JKT RUVU



KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya JKT Ruvu ya Pwani,Charles Kilinda amesema anatarajia kujiuzulu kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Kilinda alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, ameamua kujiweka pembeni na soka ili apate nafasi ya kufanya mambo mengine.

Alisema amekuwa akiinoa JKT Ruvu kwa miaka sita sasa na kwamba muda huo unatosha kwake kujiweka pembeni na kutoa nafasi kwa wengine.

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga alisema, anachopigania kwa sasa ni kuhakikisha kuwa, JKT Ruvu haishuki daraja msimu huu.

"Nataka niondoke na kuiacha JKT Ruvu ikiwa bado inashiriki ligi kuu ya Tanzania Bara,"alisema kocha huyo.

Kwa sasa, JKT Ruvu inashika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 18, ikifuatiwa na Polisi Moro yenye pointi 15, Toto African yenye pointi 14 na African Lyon yenye pointi 13.

Kocha huyo alikiri kuwa, michuano ya ligi kuu msimu huu ni migumu kutokana na timu nyingi kufanya maandalizi mazuri na kupania kutwaa ubingwa.

No comments:

Post a Comment