'
Monday, October 8, 2012
ZANZIBAR YAJITOA MICHUANO YA CAF 2012
Na Ally Mohamed, Zanzibar
WAWAKILISHI wa Zanzibar katika michuano ya Afrika mwakani, Super Falcon waliofuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika na Jamhuri waliofuzu kucheza Kombe la Shirikisho wamejitoa kwenye michuano hiyo. Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Aman Ibrahim Makungu, zimesema kwamba timu hizo zimeamua kujitoa katika michuano hiyo kwa sababu hazina fedha, ambapo kila timu ilihitaji kiasi cha dola za Kimarekani 30,000, zaidi ya Sh. Milioni 45 kwa ajili ya maandalizi ya ushiriki wa michuano hiyo. Kufuatia hatua hiyo ZFA, iko katika mazungumzo na baadhi ya klabu za Ligi Kuu ili kuona kama kuna uwezekano wa kupata timu zitakazochukua nafasi hizo. Mwaka huu Zanzibar iliwakilishwa na timu ya Mafunzo katika ligi ya Mabingwa Afrika, huku Jamhuri wakipata nafasi ya kushirki katika kombe la Shirikisho. Hata hivyo timu zote zilishindwa kufanya vizuri baada ya kuondolewa katika hatua ya mwanzo katika michuano hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment