KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, October 7, 2012

YANGA, KAGERA SUGAR SASA KUKIPIGA KESHO



Kamati ya Ligi imesogeza mbele kwa siku moja mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Kagera Sugar na Yanga iliyokuwa ichezwe leo mjini Bukoba kutokana na Uwanja wa Kaitaba kuwa na shughuli nyingine za kijamii.
Sasa mechi hiyo itachezwa kesho Jumatatu (Oktoba 8 mwaka huu) kwenye uwanja huo huo.
Mabadiliko hayo pia yameathiri mechi kati ya Toto Africans na Yanga iliyokuwa ichezwe Oktoba 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba 11 mwaka huu.
YANGA, AFRICAN LYON KUTOVAA BEJI YA MDHAMINI
Kwa vile msimu huu mdhamini mwenyewe ndiye anayegawa vifaa kwa timu, Kamati ya Ligi imeagiza Vodacom iandikiwe barua na nakala kwa klabu zote ili kujua timu ambazo tayari zimekabidhiwa vifaa hivyo zikiwemo logo na siku ambapo timu husika zilipokea.
Baada ya majibu ya Vodacom ndipo Kanuni za Ligi Kuu zitakapotumika kutoka adhabu kwa timu ambazo zitabainika kuwa zilipokea vifaa lakini hazikuvitumia.

No comments:

Post a Comment