KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, October 7, 2012

SIMBA HAKUNA KULALA, YAINYUKA JKT OLJORO 4-1



MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya  Tanzania Bara, Simba leo wameendelea kujikita kileleni baada ya kuitandika JKT Oljoro ya Arusha mabao 4-1.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kiungo Amri Kiemba aliendelea kudhihirisha kuwa moto wake hauzimiki baada ya kuifungia Simba mabao mawili kati ya manne.
Kiemba amejitokeza kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Simba hadi sasa kutokana na uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo na wakati huo huo kusaidia mashambulizi na kufunga mabao.
Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi na Felix Sunzu, aliyefunga kwa njia ya penalti.
JKT Oljoro ililazimika kumaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji tisa baada ya kipa wake, Shaibu Issa na mshambuliaji, Meshack Nyambele kutolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Amon Paul wa Mara kwa makosa ya kucheza rafu mbaya.
Bao la kujifariji la JKT Oljoro lilifunggwa na Paul Nonga baada ya beki Juma Nyoso kuanguka wakati akijiandaa kumkabili na kutoa mwanya mwa mshambuliaji huyo kumchambua kipa Juma Kaseja kabla ya kufunga bao.
Kwa matokeo hayo, Simba ilizidi kujikita kileleni mwa ligi hiyo, ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 13 baada ya kucheza mechi tano.

No comments:

Post a Comment