KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, October 11, 2012

YANGA YAWALIZA NDUGU ZAO WA TOTO AFRICAN


YANGA jana ilizinduka katika michuano ya soka ya ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa ndugu zao wa Toto African mabao 3-1 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Ushindi huo uliiwezesha Yanga kuchupa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi saba, sawa na Kagera Sugar, lakini zinatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Simba, ambayo kesho itavaana na ndugu zao wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwa, Tanga bado inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 13.
Mabao yaliyoiwezesha Yanga kutoka uwanjani na pointi zote tatu yalifungwa na Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na Jerry Tegete. Bao la Toto African lilifungwa na Saidi Mussa,
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho wakati Azam itakapovaana na Polisi mjini Morogoro, Prisons itacheza na JKT Oljoro mjini Mbeya, Ruvu Shooting itamenyana na African Lyon mjini Pwani wakati Mtibwa itavaana na Mgambo JKT kwenye uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.

No comments:

Post a Comment