KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, October 18, 2012

MIMBA YA INI EDO YAHARIBIKA




LAGOS, Nigeria
UTATA umezuka kuhusu uja uzito wa mcheza filamu nyota wa kike
wa Nigeria, Ini Edo baada ya kuripotiwa kuwa mimba yake
imeharibika.
Gazeti la Encomium la Nigeria liliripoti wiki hii kuwa, Ini amekuwa
akionekana katika hali ya kawaida, licha ya kuwepo na taarifa
kwamba alikuwa akikaribia kujifungua.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, katika hafla mbali mbali ambazo Ini
alihudhuria siku za hivi karibuni, tumbo lake limekuwa likionekana
la kawaida, hali inayozua maswali mengi.
Katika moja ya picha alizopiga hivi karibuni, Ini alionekana akiwa
amefunga mkanda mkubwa kwenye tumbo lake na kusababisha
watu kujiuliza maswali mengi.
"Ini amepoteza uja uzito wa mumewe, Philip Ehiagwina," liliripoti
gazeti hilo.
Gazeti hilo liliripoti kuwa, miezi michache iliyopita, Ini alithibitisha
kuwa na uja uzito wa miezi minane na kwamba alikuwa akikaribia
kujifungua.
"Watu walio karibu na Ini Edo wamesema, katika sherehe ya
kuzaliwa ya mwigizaji mwenzake, Stephanie Linus, Ini alionekana
kuwa katika hali ya kawaida bila ya kuwa na dalili za uja uzito,"
limeeleza gazeti hilo.
"Kama mimba yake haikuharibika, hivi sasa angekuwa kitandani
akikaribia kujifungua," lilieleza gazeti hilo.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Oktoba 8 mwaka huu, mwandishi wake
aliwasiliana na Ini kwa simu na kuzungumza na msaidizi wake,
aliyetambulika kwa jina la Edward, ambaye alisema alikuwa amelala
wakati huo.
"Sifahamu lolote kuhusu mimba yake kuharibika," gazeti hilo
lilimkariri msaidizi huyo wa Ini akisema.
"Inawezekana atakapoamka, atazungumzia suala hilo. Lakini
sifahamu lolote kuhusu taarifa hizo," alisemamsaidizi huyo wa Ini.
Gazeti hilo liliendelea kuripoti kuwa, liliwasiliana na Ini mara kadhaa
kwa njia ya simuna ujumbe wa maandishi, lakini hakuwa akipokea
wala kuzijibu.
Ujumbe uliotumwa na gazeti hilo kwa Ini ulisomeka hivi: "Tulikupigia
simu, lakini Edward alisema ulikuwa umelala.
Kuna taarifa hapa kwamba, mimba yako imeharibika na
tungependa kupata ukweli kutoka kwako kabla ya kuchapisha
habari hizi."

No comments:

Post a Comment